Sasa hivi unaweza kuona matokeo kwa asilimia. Bonyeza hapo kwenye (View results) kwa kila ballot utaona...Itaweza kuonekana hivi kwa masaa mawili...wakati bado unaweza piga kura kwa wale ambao hawajamalizia kupiga kura..Baada ya hapo kura zitafungwa na tutakamilisha zoezi hili na kuweka matokeo yote hapa hadharani kesho Tumeachia muone wenyewe kwa vile kuna watu mwaka jana walilalamika na kushangaa iweje vipi blog fulani haijashinda wakati ina watu wengi wanaosoma katika mji fulani? Jibu hatuna sisi ila ballots ndio zinajieleza zenyewe.....Baada ya kutengeneza hizi form sisi hatuna uwezo wa kuongeza au kupunguza kura..Mwaka jana nilijaribu kuweka results hadharani kumbe haiwezi kufanya hivyo mara baada ya muda kuisha wa kupiga kura....
Ila tukiangalia tunaona kuwa kura nyingi sana zimepigwa na watu ambao hawako Tanzania...Sasa tunaloona na kufikiri ni kuwa labda kwa vile watu wengi Tanzania wanatumia simu ndio imekua vigumu lakini watu wengi pia wanatumia simu nchi za nje kusurf the net na waliweza kupiga kura. Labda ni network connection ndio shida, au labda watu walioko Tanzania wanahitaji uhamasishwaji wa aina nyingine ili kushiriki katika mambo mbali mbali..Anyway..Hatujui sababu ni ipi lakini karibu 75% ya watu waliopiga kura mwaka huu wako nje ya Tanzania.
Hongera kwa wote mlioshinda..lakini kumbuka wote ni washindi
2 comments:
Thanks a lot kwa kweli na huu ni mwanzo mzuri wa blog zetu...!! Kwa woote mloshow support mpaka kuifikisha hapo nolniz.blogspot.com na wadau wooote WEUSI we thank you
Shukurani mpendwa, ila matokeo hayo ya `asilimia ' yameondoka mapema, maana wengine wikiend hatupo makazini na mitandano ya majembe tunayapatia kazini.
Hata hivyo pole sana na jopo lako,najua ilikuwa kazi ngumu, lakini hatimaye mumefikia mwisho wake.
HONGERA SANA KWA WASHINDI, NA WALIOSHINDWA SIO HOJA NI MTIZAMO TU, NA MWANYA WA KUPATA WAPIGA KURA, KILA MMOJA NI MSHINDI KATIKA BLOG YAKE
Post a Comment