Lala Salama. Leo ni Siku ya Mwisho Kupendekeza Majina

Tunawashukuru watu wote waliochukua muda wao na kujaza form za blogs zao au blogs za watu wanaopenda washiriki katika shindano hili.

Ukweli ni kuwa miezi miwili ya kupendekeza majina iilikua mingi sana lakini hii yote ni kwa sababu hatukutaka malalamishi kama ya mwaka jana ya watu kusema hawakupata taarifa au hawakupata muda wa kutosha. Ila kwa idadi ya watu waliojaza hii form mwaka huu na kutoka katika nchi nyingi sana, tunaamini kuwa ni watu wengi sasa wanaofahamu hili shindano sasa. Hivyo mwakani Mungu akitujalia  tutajitahidi kupunguza muda wa kupendekeza uwe mwezi mmoja au hata week mbili tu.

Wow! Mwaka huu tunashukuru kuwa watu wameitikia wito na kujaza form. Ukiangalia map ya watu walioingia humu hata nchi nyingine huwezi amini kuna watanzania wanaishi humo au kuna watu wako interest na hili shindano katika nchi hizo.  Tunashuku na tunafurahi kuwa watu wakiingia wanaangalia na directory list yetu na kuona blog za Tanzania. 

Kingine ninachopenda kusema mimi binafsi ni shukurani zangu kwa watu wote kwa vile mwaka huu negatives comments hazikuwa nyingi kama mwaka jana. Mwaka huu wale wachache wanaokua katika kila jamii na kuwa na lao baya la kusema hata katika kitu kisicho na lengo baya  walikua wachache sana sana sana. Shukrani kwa hilo...

Tunachofurahia kingine katika mafanikio ni jinsi blog mpya zilivyofunguliwa. Blog ni nyingi sana mpya na hii ndio mafanikio na moja ya malengo ya blog hii na shindano letu pia..

Mwaka huu hii form imejazwa mara nyingi sana. Zimezidi  expectations zetu kwa kweli. Ingawaje naweza kusema spam (wale waliokua wanajaza form zaidi ya mara tano) kwa wakati mmoja ni kama 1000 hivi lakini still kuna zaidi ya 5500 ambazo watu hao walikua wanajaza mara moja tu kwa siku na kujaza form mara moja au mbili tu.

Ila tulichogundua ni kuwa watu wengi sana wanaotembelea hii site ni kwa kutumia simu. Hivyo tunachofikiria huko mbeleni tutajitahidi kutengeneza form ambazo zinaweza kusomeka kwa kutumia simu..

Majina tutayaweka leo ya watu wote waliopendekezwa. lakini itachukua muda kwa watu zaidi ya watano kuprocess data zote na kuangalia kuwa site zilizopenendekezwa katika kila kipengele zinastahili. Hii yote ni ili kuwa fair kwa kila mtu. Hivyo kama sheria zetu zinavyosema Kura zitaanza kupigwa June 15th. Tutaweka majina ya hayo tarehe 13 na badge zitapatikana hapa muda huo. Kama utapenda kuchukua badge hiyo tafadhali utaiona tarehe hiyo..Kura zitapigwa kwa week mbili tu.

Shukrani

No comments: