Tanzanian Blog Awards 2013

Tumekua tukipokea email nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wakituulizia kuhusu jinsi ya kushiriki katika shindano la mwaka huu na wengine kututumia blog zao katika email yetu ili tuweke majina yao katika shindano hili. 

Kama tulivyosema hapo mwanzoni mwa mwaka huu ni kuwa tuliamua kulihamishia shindano letu kwenda mwezi wa nane (August) kutoka na maombi ya bloggers wengi ambao ni wanafunzi walituambia kuwa katika kipindi kile huwa wengi wapo katika mitihani yao ya shule na wengine huwa ndio kipindi cha kumalizia papers na researches zao, hivyo ndio tukaa na kujadiliana na kuona ni bora kuliweka shindano hili katika mwezi wa nane.

Na pia wengine walisema muda tunaotumia kukusanya majina ya washiriki na wa kupiga kura ni mrefu sana.  Hivyo tulivyokaa na kuangalia haya maoni pamoja na maoni mengine tuliamua kukubaliana na maoni haya kwa wakati huu. 

Hivyo kuanzia sasa hivi shindano hili litakua mwezi wa nane na pia tutakua tukikusanya majina ya washiriki katika shindano hili kama ifuatavyo hapo chini. 

Nomination accepted 
August 17th - 30th, 2013 (For Two Weeks) 
(Form zitawekwa hapa na majina ya washiriki yatapokelewa) Angalia FAQs yetu ujue ni blog gani zinaruhusiwa kushiri. 

Panel Selection 
Sept 1st - 7th, 2013
Voting 
September 8th - 14th, 2013  
 
Winners announced
September 15th, 2013

No comments: