Jina la Blog Kubadilika

Kama tulivyowaambia hapo awali kuwa blog hii imepata nyumba mpya..Award yetu itabakia hivi hivi kwa jina la Tanzanian Blog Awards...lakini award hii sasa hivi itakua chini ya Bloggers Association of Tanzania. Sheria nyingi za shindano zitabakia hivi hivi lakini kwa vile itakua chini ya association itakua ni kwa kujoin kuwa member ili kushiriki katika shindano hilo kwa wanaopenda
  
Link ya www.tanzanianblogawards.com itaisha hivi karibuni hivyo hii kwa maelezo mengine kama hutaweza kusoma post mpya kwa kwenye platform ya blogspot basi check facebook page yetu mpaka hapo tutakapopokea link ya website ya Bloggers Association of Tanzania. 

Tulipokeaga maombi ya bloggers wengi ambao ni wanafunzi na walishauri kuwa tupeleke mbele shindano hili kwa vile kipindi hiki ni cha wengi kushughulikia projects/paper zao na kujiandaa kwa mitihani hivyo tulikua tumeshafikria kuhamisha shindano hili na kulipeleka mwezi wa nane.  Na pia kwa vile blog hii inaenda kumilikiwa na associassion na itabadilika link hivi karibuni basi ni vizuri tuanze kwa mwaka huu kuhamisha shindano hili katika mwezi huo ili kupunguza usumbufu wa watu wengi ambao watakua hawajui link mpya.. Angalia FAQ utaona tarehe za mwaka huu...

Shukrani

No comments: