Kushiriki kwa shindano letu

Tunaamini mwaka huu kutokana na watu walivyojaza form za kushiriki katika shindano letu mpaka sasa hivi ni kama aslimia (540%) zaidi ya mwaka jana, hivyo tunaamini watu wengi zaidi ya mwaka jana wanafahamu kuhusu shindano hili. Na pia tunaamini bloggers waliopendekezwa blog zao kushiriki wote wanafahamu kuhusu shindano letu. Hivyo kwa mwaka huu tafadhali tambua kuwa tutaweka majina ambayo yamependekezwa week hii na week ijayo. Na kutakua na week moja ya kuchugua nomination badges. Kama ukiona jina la blog yako na wewe hutaki kushirikishwa tafadhali tuandikie sisi tutaliondoa. Mwaka jana watu wengine walilalamika kwanini tumewapa habari baadhi ya bloggers tu na tukaacha wengine. Haikua nia yetu kufanya hivyo bali tulijitahidi sana kuwasiliana na kila blogger ambaye tulikua na email yake na kama unavyojua mwaka jana tulipata shida sana ya kuwasiliana na bloggers wengi kwa vile emails walizoandika kwenye blogs zao nyingi hazipo active na nyingine zina auto responses tu.  

Sasa sisi mwaka huu tumekaa na kufikiria hili suala kwa undani na tumeamua kuwa mwaka huu hatutawasiliana na blogger yeyote. That is right....HATUTAWASILIANA na blogger yeyote kumfahamisha kuhusu kushiriki katika shindano letu. Kama umependekeza blog ya mtu please mwambie hivyo kama hataki basi mtuandikie tuondoe jina lake. Mara tukishaweka majina hapa  na kuanza voting process hatutaondoa jina la blog yeyote. 

Na hii ni kusema kuwa baada ya mashindano tutatangaza washindi na kama mtu atataka badge ya kuonyesha kuwa alishiriki au alishika nafasi fulani katika shindano letu au anataka cheti cha kuonyesha kuwa alishiriki pia itabidi utuandikie . Mwaka huu tutacustom order vyeti hivyo sio kama mwaka jana tulitengenza kwa watu wote bila kujali utakihitaji au la. Ilikua kazi sana kuwatumia wengi kwa ajili ya email address ambazo zilikua zipo au hazipo. Na pia tunajua kuna watu wanahitaji vyeti kuengeza katika portfolio zao na wengine hawahitaji hivyo vyeti kwa vile hawahitaji kutumia katika kitu chochote. Hivyo kupunguza gharama mwaka huu shindano likiisha tutatangaza muda wa watu kuchukua badges zao na pia muda wa kuchukua vyeti vyao..

Shukurani

No comments: