Tanzanian Blog Awards Newsletter

Tunafurahi kuwafahamisha kuwa tumeanzisha newsletter mpya ya Tanzanian Blog Awards kwa ajili ya Public Relation. Hii newsletter itakuwa at most inatumwa kila week kwa bloggers (ya watu wasio na blogs inakuja hivi karibuni)

Umuhimu wa hii newsletter ni kusaidia kurahisisha habari mbalimbali muhimu ambazo huwa si rahisi kuwafikia bloggers wengine.

Na upande mwingine nakumbuka tulivyoanzisha hii site tulikua hatujui blogs nyingi za watanzania na hatukujua kuwa ni bloggers wapi au wangapi watakao kubali kuweka tangazo letu kwenye blog yao licha ya hata kupata muda wa kulisoma tu. Na kweli tulivyotuma matangazo yetu kwa wale bloggers wachache tuliokua tunawafahamu kwa wakati ule wengine walukubali kuweka tangazo letu na wengine hawakukubali. Haikua big deal kwangu mimi kwa vile nilishafanya kazi kwenye community newspaper na nilielewa sio kila habari inayopokelewa basi  ni lazima itachapishwa. Anyway kwa upande wa mtu ambaye anajaribu kutafuta watu wa kumsaidia kujitangaza halafu hao wachache anao wafahamu wasipost  inakua vigumu na taabu sana kujulikana mwenyewe kama hatatumia njia nyingine. Wengine kwa vitendea kazi vigumu na vichache walivyonavyo basi wanakua limited kuanza kutafuta nani mwingine wa kumweleza kuhusu blog yake na mwisho wa yote ndio huo tunaona blogs nyingi za kitanzania zinaisha katikati pamoja na kuwa na mambo mazuri na ideas nyingi nzuri sana tu.

Hivyo kwa kufikiria hayo yote tumeamua kuja na hii newsletter ambayo kama mtu ana blog yake mpya au tangazo lake lolote na hajui ni blog gani ya kuwatumia au hata akiwatumiwa wataweka au la basi ni heri atutumie sisi tutakusanya habari hizo kwa week moja na kuzifoward mara moja kwa mabloggers wote. Watakaoona habari yako inaendana na wasomaji wa blog yake basi kama watataka watapost na watakaaoona haiendani na wasomaji wa blog yao basi hawataposti lakini atleast habari yako itawafikia bloggers zaidi ya mia kwa mara moja

Kazi ya kublog ni kubwa sana na sasa ukiongeza kusoma comments ka wale wanao moderate, kutafuta habari za kuweka halafu uje kwenye emails za matangazo ya kawaida tu inakua vigumu sana kwa blogges wengine ndio maana wengine wanaishia hata kutokusoma emails zote zinazowafikia kila siku. Natumaini hii itapunguza msongamano wa emails na kuengeza ufanisi katika mambo mengine yanayohusiana na blogs zao..

Bloggers kuna wachache nina email zenu mara ukipokea newsletter ya kwanza tutakayoituma basi unaweza kujiondoka katika hilo group kama hutapendelea kupokea tena. Na kwa wengine ambao mtakua hamjapokea email kutoka kwetu basi naomba mjiandikishe kwa kutumia hiyo form iliyoko katika upande wa kulia hapa. Naomba ieleweke hii newsletter ya kwanza sio special kwa baadhi ya bloggers tu bali ni kwa wale wachache niliobahatika kuwa na emails zao na kila blogger popote pale alipo anaruhusiwa kuingia katika list yetu kama atapendelea kupokea hii newsletter.

Na kwa wale watu wenye blog mpya au matangazo yeyote mnayooona yanahitaji kuwaafikia watanzania wengi popote pale walipo basi mtutumie sisi tutayakusanya na kutuma mara moja kwa week. Kama tangazo lako ni time sensitive tutajitahdli kulituma siku hiyo hiyo tunapolipokea ama sivyo basi tutaliweka mpaka siku ya kutuma matangazo yote. 

Nadhani itasaidia wengi ..and as always press release sio lazima. Participation ni kwa wewe mwenyewe kupenda kusaidia wengine na kama habari unayoipata haihusiani na blog yako sio lazima kuposti....

3 comments:

aboodmsuni said...

Great thing, tunangoja ufanisi wakeGreat thing, tunangoja ufanisi wake

Anonymous said...

idea nzuri sana, mnafanya kazi nzuri sana

Anonymous said...

It is a excellent ideas specially to individuals new to blogosphere, short and correct information… Many thanks for sharing this a single. A should examine report.