Wako wapi?

Je unajua kijana yeyote ambaye ni mtanzania mwenye umri kati ya miaka 12 – 18 mwenye blog? Mpaka sasa hivi nilipokua naandika chini majina ya blogs yaliyopendekezwa kwenye shindano letu bado sijaona blog ya yeyote iliyopendekezwa ya vijana wenye umri huo. Je ni hizo blog zipo lakini watu hawajazipendekeza tu au hazipo kabisa?

Umuhimu wa kushawishi vijana waingie katika hii fan ya kublog ni mkubwa sana na mzuri sana? Najua nchini kwetu kutokana na blog ile ya UTAMU watu wengi wamechukulia blog kuwa ni kitu ambacho ni chakudhalilisha watu tu au ni kazi za waandisha wa habari tu lakini ukweli ni kuwa blogs ni kwa kila mtu na kwa vijana zina saidia sana mtu kufahamu mapenzi ya kitu anachotaka kufanya akiwa mtu mzima mapema sana.

Wengi wetu tulivyokua tunashoma shule za msingi na secondary haya mambo yalikua hayapo. Wengi tulikua tunakwenda shule na kufaulu vizuri lakini mpaka tuna miaka 19 hatujui vizuri ni nini hasa tungependelea kufanya katika maisha yetu. Information zilikua sio nyingi na zilizopo zilikua kutoka kwa walimu au magazeti kutoka kwa wenye bahati ya kuwa na wazazi wasomi.

Ulimwengu tunaoishi sasa hivi ni rahisi sana kupata na kujifunza mambo mengi kupitia katika mitandano. Na jinsi ya kuingia kwenye mitandao sasa hivi sio vigumu sana ukizingatia watu wengi wanatumia simu kuingia kwenye mitandao. Niliona tweet moja kutoka kwa Mr. Chahali inasema “Upatikanaji wa mtandao katika vilongalonga watishia uhai wa maduka ya huduma za mtandao (internet cafes) nchini”. Hivyo vijana wengi sasa hivi wenye kupennda kuwa na blog haitakua vigumu sana.

Mwezi wanne rafiki yangu mwenye mtoto wa miaka 6 aliniambia anamsaidia mtoto wake kutengeza kitabu ambacho mtoto huyo anakiandika. Nilishangaa mtoto mdogo hivyo anaandika kitabu? Rafiki yangu huyo akaniambia ni assignment wamepewa shuleni wakati wa spring break kuwa wakirudi shuleni waandike kitabu cha jinsi walivyospend spring break zao. Nilivutiwa sana na kitendo hicho kwa vile hiyo itawasaidia watoto kujua kumbe hivi vitabu wanavyovisoma kila siku vinaandikwa na watu kama wao. Hata mtu yeyote akitaka kuandika kitabu siku moja basi ni kukaa chini na kuweka mawazo yake pamoja na kuandika. Ukianza kufanya kitu mara kwa mara inaongeza uzoefu na kujiamini hata siku moja ukafanya mambo makubwa kuliko hayo unayozoea kufanya kila siku.

Ni vizuri tukiwahamasisha wadogo zetu, watoto wetu, nieces na nephews kutumia muda wao wanaoingia online vizuri. Blog zinasaidia sana kwa vijana wadogo kujua shauku zao ziliko mapema sana. Blogs pamoja na kuwa zinapeleka habari haraka sana akini sio kila blog lazima iwe ya habari. Unaweza kuanzisha blog ya science, technology, sanaa, utamaduni, Kiswahili, vichekesho, michezo, maarifa ya nyumbani n.k.

Pamoja na kuwa utakua unazungumzia mambo unayoyapenda lakini unajifunza mambo mengi sana pia unapokua na blog kama kuwa na mawasiliano mazuri kati yako na wasomaji wako (communication skills), kuongezea ujuzi wako wa kuandika (writing skills), inakusaidia kuongeza uwezo wako wa kuhariri (editing skills), inakuengezea ujuzi kwenye technology, inakufundisha kufanya utafiti (hii itakusaidia sana ukiwa katika elimu ya juu) au hata kama utaamua kuishia elimu katika level yeyote, itakuengezea ujuzi wa kujua jinsi ya kupublish, kuorganize mambo yako au kuorganize groups, fund raising na mambo mengi tu. Na vitu viwili vikubwa zaidi itakayokuengezea ni kujiamini katika mambo yako mengi unayofanya na kuwa na marafiki mbalimbali au hata nchi mbalimbali wanaopenda mambo unayoyafanya.

Juzi kwenye CNN walikua wanamhoji mtoto ana miaka 11 amezanzisha empire ya mapishi. Pia food channel imeshamtaka huyo mtoto ili wamtengenezee show yake ya mapishi. Huyo mtoto anasema alikua anapenda kupika toka akivyokua mdogo sana na alianza kurekodi picha za jinsi anavyotayarisha mapishi yake na kuweka kwenye youtube. Kutoka huko kwenye youtube ndio biashara yake ya mapishi ikaanza. Kama mtu unakipaji na unakaa nacho ndani nani atakuona au utajuaje kuwa unakipaji kama hutafanya mazoezi au kuwaonyesha watu unachojua? Siku hizi kwa technologia iliyopo sio lazima usubiri kwenda kwenye audition. Mambo mengi ni wewe utakavyojitahidi kujionyesha kwa watu na ulimwengu mambo unayoyajua.

Pamoja na kutembelea blogs za watu kusoma mbalimbali na kuacha comments kila siku (sio vibaya kufanya hivyo) lakini hata wewe unaweza kuwa na blog na watu wakaja kuizoma. Unaweza kuwa na blog pia kama watoto wengine wa nchi zilizoendelea. Sio kufollow blog zao tu kila siku hata wewe unaweza kuwa na blog yako na wao wakafolllow blog yako. Ungejua kuwa kuna watu wengi wanataka sana kujua mambo unayojafahamu pia kama wewe uanvyotaka kufanhamu mambo ya watu wengine.

Mimi (mwandishi wa blog hii) nipo kwa yeyote yule kama kuna kijana yeyote (12-18) yrs old anahitaji msaada wa kuanzisha blog au idesas email ipo hapa....Niandikie mimi natakusaidia kadri nitakavyoweza kuhakikisha una blog yako ya maana. Na pia nitakusaidia kuitangaza.

3 comments:

Aidan Leonce (iDone Skales) said...

SALAAM
JAAMANI MIMI NIPO HAPA NAITWA AIDAN LEONCE NINA MIAKA 14,(BUKOBA) TANZANIA. NINASOMA BUKOBA SECONDARY FORM TWO,NILIANZA KUWA MPENZI WABLOG MDA MREFU SANA NA NILIFURAHISHWA SANA KUSIKIA KUWA BLOG ZILIKUWA ZINATENGENEZWA BURE, BASI NA MIMI NIKAJARIBU KUTENGENEZA NIKAFANIKIWA KUTENGENEZA BLOG YANGU YA KWANZA ITWAYO HTTP://AIDANLEONCE.BLOGSPOT.COM/ HII NDO BLOG YA KWANZA KABISA KWANI NILIKUWA NA IBADILISHA KILA SIKU MPAKA IPENDEZE KWENYE BLOG HII NINA POST HABARI ZA MICHEZO /MUZIKI NA MAMBO YA DUNIA MBALIMBALI BLOG HII PIA IMECHAGULIWA KUSHIRIKI KWENYE MASHINDANO YA TANZANIA BLOG AWARDS HAYA NI MAFANIKIO MAKUBWA KWANI HATA SASA NIKIANGALIA WAGENI WANAOTEMBELEA BLOG YANGU NASHUKURU MUNGU NI WENGI SANA KWA SIKU HATA WATU 80 TOKA NCHI MBALIMBALI,BAADA YA KUWA NAJIFUNZA DESIGN BLOG NATAKA KUFUNGUA KAMPUNI YA KUTENGENEZA BLOG ZENYE QUALITY NZURI KWANI NIMEWEZA KUFUNGUA BLOG NYINGINE MBILI HTTP://TZTUBE.BLOGSPOT.COM/ KWENYE BLOG HII KUNA VIDOE TUU ZA WASANII WA KITANZANIA. HTTP://GLOBETECHNO.BLOGSPOT.COM/PIA BLOG HII BADO SIJAANZA KUPOST LKN BLOG HII ITAKUWA NA HABARI ZA SCIENCE NA TECHNOLOGY.PIA SASA NIKO NA WEB YANGU MBILI YA KWANZA NI YA KAMPUNI ITWAYO AIDAN199. HTTP://AIDAN199.TUMBLR.COM/ NA NILIKUWA KWENYE MPANGO YA KUFUNGUA SOCIAL WEBSITE LAKINI HAINA DOMAIN NAME INAITWA HTTP://GLOBEMUSIC.WEBS.COM/

Admin said...

Aidan tunakupa hongera sana kwa blog yako kuingia katika shindano hili. Mimi binafsi nimefurahia kuona umefungua blog yako baada ya kufahamu kuwa hakuna malipo yeyote yanayohitajika ili uweze kuwa na blog. Na pia nimefurahishwa kusikia kuwa katika umri huo mdogo umeweza kuwa na blogs nzuri hivi. Ni kitu cha kujivunia sana na ujue kuwa pamoja na kuwa utakua unachoka sana katika kuhakikisha blog zako zina mambo mazuri na vitu vingine vingi lakini utajifunza mambo mengi sana sana na wengi watajifunza kutoka kwako na ninatumaini vijana wengine wadogo watafuata mfano wako.

Tunakutakia mafanikio mema katika blog zako.

Anonymous said...

I don't disagree with you.