Umuhimu wa kuweka Meta Tags katika kila blogger post

Meta tags ni kitu kidogo kuweka lakini kinasaidia sana katika kuongeza Search Engine Optimization (SEO). Kila mtu anataka kuengeza idadi ya watu wanaosoma au kutembelea blog yake. Kuna vitu kadhaa unaweza kufanya na vikakusaida sana kuengeza idadi ya watu wanaopitia katika blog yako. Kitu ambacho ni muhimu ukiweza kuweka blog yako ni meta tags ambazo zinasaidia sana watu kupitia blog yako kwa maneno uliyoyaweka kwenye blog yako. Ingawaje watu wengi wanaweza kuweka meta tags katika blog zao na kuna blog templates nyingine zina meta tags tayari hivyo wewe ni kujaza tu maneno makuu unayoyaona yanahusianan na blog yako lakini ukumbuke hayo ni maneno makuu. Ingawaje yanatofauti sana na yule ambaye hajaweka lakini ukiweka meta tags za maelezo pia zinaongeza sana tofauti kati ya yule mweye nayo na yule asiyenayo. Kam ziko blog mbili zina maelezo sawa na ya kwako umeweka meta tags za maelezo ya kwako itaweza kuonekana mapema na pia inasaidia sana kuonekana kwenye indexing. Hivyo kuna njia moja ya kutwist kidogo na kuweza kuweka blog yako kwenye nafasi ya juu kuonekana zaidi.

Jinsi ya kufanya

1. Nenda kwenye Dashboad ya blog yako.

2. Ingia kwenye Design.

3. Nenda kwenye Edit HTML

4. Back up template yako kabla hujafanya chohote...Unaweza kukopy na kupaste kwenye note pad au kudownload kwenye hard drive yako.

5. Tafuta haya maneno kwenye template yako. Kwa urahisi tumia Ctrl+F kuyatafuta....

< title>< data: blog. pageName/> | < /title >

6. Copy haya maneno hapa chini na uweke china ya hiyo line hapo juu.

< meta expr:content='data:blog.pageName' name='description'/ >


Basi save na umemaliza.

Sasa hii ina maana mtu yeyote atakayekua anasearch kwenye blog yako kwenye google au search engine yeyote ataona jina la blog yako na maelekezo ya kitu anachotafuta kwenye description kutoka katika post yeyote ile. Na utawapita wale wanaoonyesha neno moja moja tu. Sasa maelezo yako kama ni hayo anayotafuta atavutiwa kuingia na kusoma zaidi kwa vile mtari mzimautakua umeonekana hapo.

Ingawaje ukishaweka itachukua kama masaa kadhaa kabla ya kufanya kazi.

Hizi tag kama utaweka vizuri zitaafanya kazi kwney blogger ila nadhani zinaweza kufanya kwenye platform yeyote ile kwa vile zina generate search kutoka kwenye title.

No comments: